Paul Manjale
NAHODHA Mbwana Samatta na Farid Mussa hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Taifa Stars ambacho kesho Jumanne kitashuka kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam kucheza na Burundi kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya shirikisho la soka duniani ,FIFA.
Kukosekana kwa wachezaji hao wanaosukuma kandanda la kulipwa barani Ulaya kunatokana na Kocha mkuu wa Taifa Stars,Salum Mayanga kuamua kuwatumia wachezaji wanaocheza ligi kuu bara pekee.
Wakati huohuo Mayanga amemteua Himid Mao Mkami kuwa nahodha mkuu kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Burundi huku msaidizi wake akiwa ni Jonas Mkude.
0 comments:
Post a Comment