Francis Lameck
Unguja
Ligi kuu soka ya Zanzibar msimu wa mwaka 2017-2018 itashirikisha vilabu 12 pekee kwa Zanzibar nzima na itakuwa ikichezwa kwa kanda mbili tofauti kwa kanda ya Pemba na kanda ya Unguja.
Kwa mujibu wa Makamu wa Urais wa ZFA Pemba, Ali Mohammed amesema
baada ya kupatiwa uanachama wa kudumu kutoka Shirikisho la soka Barani Afrika
wametakiwa kupunguza timu na kubakiwa na timu 12 tu kwa msimu ujao.
Wadau wengi wa soka Visiwani Zanzibar wanahamu ya kujua vipi
vilabu hivyo 12 vitapatikana ambapo jukumu hilo kwasasa wamepewa umoja wa
vilabu kwa kukaa pamoja na vilabu vyao kwa kujadili mfumo gani watumie ili
zipatikane timu hizo 12 kisha kuwarejeshea tena kamati tendaji ya ZFA kama walivyokubaliana.
Aidha kamati tendaji wataangalia mfumo ambao wameletewa na
umoja wa vilabu kama watakuwa na uwezo wa kutoa ufafanuzi wataelezea na endapo
kamati tendaji wakishindwa, litaenda kuamuliwa na kutolewa ufafanuzi katika
mkutano mkuu ambao unatarajiwa kufanyika April 8 na 9, 2017 huko Kisiwani
Pemba.
Kwa upande wa ligi daraja la kwanza vilabu vitakavyoshuka msimu
huu pamoja na vile ambavyo vitakavyobakia katika daraja hilo vitashiriki hata
kama vitafika zaidi ya 30 wakati huo huo daraja la Pili Taifa linatarajiwa kuvunjwa.
Pia msemaji wa Zfa taifa amezungumzia namna ya
upatikanaji wa pasposti za wachezaji wa Zanzibar ambao wataitumikia timu ya
taifa ya Zanzibar nakusema wachezaji watakaotumika kwenye timu ya taifa ya Zanzibar ni wale wenye paspoti ya Mzanzibar.
0 comments:
Post a Comment