728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, March 26, 2017

    Hizi hapa habari kubwa za usajili kutoka barani Ulaya leo Jumapili Machi 26,2017

                                                                         Kylian Mbappe

    Paul Manjale.

    Messi:Lionel Messi ameripotiwa kuwa mstali wa mbele kuzuia kuuzwa kwa beki,Jordi Alba kwenda Manchester United.Messi anadaiwa kuwa hajafurahishwa na namna ambavyo Barcelona imeshindwa kuziba pengo la Dani Alves katika beki ya kulia hivyo hataki kuona tena jambo hilo likitokea  katika nafasi ya beki wa kushoto anayocheza Alba.(Diario Gol)

    Mbappe:Monaco imesema itamruhusu kinda wake mahiri,Kylian Mbappe kuondoka Stade Luis II ikiwa tu itapokea ofa ya £130m.Msimu huu Mbappe,18,amejikuta akitakiwa na vilabu vikubwa vya Hispania na England baada ya kufunga mabao19 na kupika mengine 11 katika michezo 32.(Daily Express)

    Perisic:Kocha wa Manchester United,Jose Mourinho anataka kukiimarisha kikosi chake kwa kumsajili winga wa Inter Milan,Ivan Perisic anayedaiwa kuwa na thamani ya €40m.Perisic,26,ana mkataba na Inter Milan mpaka Juni 2020.(La Gazzetta
    dello Sport).

    Dahoud:Liverpool imeripotiwa kuwa bado haijakata tamaa ya kuiwania saini ya kiungo mahiri wa Borussia Monchengladbach,Mahmoud Dahoud,21licha ya staa huyo kuvutiwa zaidi na mpango wa kujiunga na Borussia Dortmund. (Daily Star)

               
                                                                        Mahmoud Dahoud

    Rose:Kocha wa Manchester City,Pep Guardiola ana matumaini makubwa ya kumsajili beki wa kushoto wa Tottenham,Danny Rose, 26,anayedaiwa kuwa na thamani ya £50m.(Daily Mirror)

    Wilshere:Kiungo wa Arsenal,Jack Wilshere, 25,anafikiria kujiunga na AC Milan ya Italia katika dirisha lijalo la usajili baada ya kushauriwa kufanya hivyo na kiungo wa zamani wa England,David Beckham.Kwa sasa Wilshere anaichezea Bournemouth kwa mkopo.(Daily Mail)

    Koeman:Kocha wa Everton Mholanzi,Ronald Koeman amedaiwa kuwa atawaomba matajiri wa timu hiyo wampatie kitita cha £100m ili kukijenga upya kikosi hicho ikiwa nyota wake wawili Romelu Lukaku, 23 na Ross Barkley, 23,wataondoka mwishoni mwa msimu huu. (Daily Mirror)

    Tadic: Vilabu vya Juventus na Napoli vimeonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Southampton,Dusan Tadic, 28,ambaye kwenye mkataba wake kuna kipengele kinachomruhusu kuuzwa kwa £13m.(TuttoMercatoWeb - in Italian)

    Mourinho: Kocha wa Manchester United,Jose Mourinho amesema hakwenda Zagreb kuutazama mchezo  wa Croatia dhidi ya Ukraine kwa ajili ya kusaka wachezaji wapya bali alikwenda kuwasalimia marafiki zake na kufurahia hali ya hewa. (Sportske Novisti - in Croatian)

    Casillas:Marseille inataka kufanya usajili wa kushtukiza kwa kumsajili kipa namba moja wa Porto ya Ureno,Iker Casillas,35 kwa kumpa mkataba wa miaka miwili.(A Bola)

    James:Staa wa Real Madrid,James Rodriguez  ameibuka kuwa chaguo la kwanza la Liverpool kwenye usajili wa msimu ujao ikiwa timu hiyo itafuzu kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu ujao.(Mirror)

    Kroos:Kiungo wa Real Madrid,Toni Kroos amesema hana mpango wa kwenda kucheza soka China wala Marekani na badala yake angependelea kuendelea kufurahia soka lake kwa kubaki Ulaya na kucheza kwenye ligi kubwa.Kroos ana mkataba na Real Madrid mpaka mwaka 2022.(Faz Sport)

    Costa:Mshambuliaji wa Chelsea,Diego Costa amefichua kuwa anavutiwa sana na maendeleo yaliyopigwa na vilabu vya Ufaransa katika siku za hivi karibuni na kuongeza kuwa huenda siku moja akashawishika kwenda kucheza soka nchini humo.(Téléfoot)

    Di Maria:Raisi wa Real Madrid,Florentino Perez ameripotiwa kuwa hivi karibuni alifanya mazungumzo ya ana kwa ana na winga wa zamani wa klabu hiyo Angel Di Maria,27, kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kumsajili kwa mara nyingine tena.(Don Balon)

    Schmeichel:Arsenal inafikiria kumsajili kipa wa Leicester  City,Kasper Schmeichel katika kipindi hiki ambacho kocha wake,Arsene Wenger anajiandaa kusaini mkataba mpya wa miaka miwili wa kubakia klabu hapo.( Mirror )




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Hizi hapa habari kubwa za usajili kutoka barani Ulaya leo Jumapili Machi 26,2017 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top