Paris,Ufaransa.
WARENO wawili wajivuni, Cristiano Ronaldo na Jose Mourinho ndiyo wanasoka waliovuna mkwanja mrefu zaidi msimu wa 2016-17, hii ni kwa mujibu wa jarida la michezo la Ufaransa, France Football.
France Football limesema,Ronaldo,31, ameibuka kinara baada ya kuvuna Euro Milioni 87.5 ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani Milioni 95.3 na kumbwaga mpinzani wake wa karibu,Lionel Messi aliyevuna Euro Milioni 76.5.
Nafasi ya tatu imechukuliwa na Neymar Jr aliyeingiza Euro Milioni 55.5 mbele ya Gareth Bale aliyevuna Euro Milioni 41.Nafasi ya tano imeenda kwa Ezequiel Lavezzi wa Hebei Fortune ya China aliyevuna Euro Milioni 28.5.
Wakati Ronaldo akikimbiza kwa upande wa wachezaji,Kocha wa Manchester United,Jose Mourinho ametajwa kuwa ndiye kocha aliyeingiza mkwanja mrefu zaidi kuliko makocha wote duniani baada ya kuvuna Euro Milioni 28.
France Football limeongeza kuwa vipato hivyo ni kutokana na mishahara,bonasi pamoja na matangazo ya kibiashara.
0 comments:
Post a Comment