Faridi Miraji
Kundi lililosalia la wachezaji wa Simba limeondoka leo kuelekea mkoani Kagera kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Wachezaji hao wameondoka na ndege aina ya Bombadier ili kuwahi mazoezi na wenzao, kabla ya mechi hiyo.
Makamu Rais wa Klabu ya Simba amesema kuwa walioondoka ni wachezaji waliosalia kwa ajili ya kuzitumikia klabu zao za taifa.
Wachezaji hao ni Ibrahim Ajibu, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Mzamiru Yassin, Abdi Banda, Jonas Mkude, Said Ndemla, na Shiza Kichuya ambao waliichezea timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars kwenye mechi mbili dhidi ya Botswana na Burundi.
Mwingine ni Laudit Mavugo aliyeichezea timu ya taifa ya Burundi ambaye pia ameungana na wenzake kwenda kuungana na kundi lililotanguliwa awali.
Simba itakuwa Kanda ya Ziwa kucheza mechi tatu mfululizo, kwani baada ya kucheza dhidi ya Kagera Sugar, itakwenda mkini Mwanza kucheza dhidi ya timu za Mbao FC na Toto Africans.
0 comments:
Post a Comment