728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, March 26, 2017

    Baada ya miaka 11 ya vichapo 58 hatimaye Andorra wapumua


    Andorra.

    HATIMAYE Andorra imemaliza gundu lake la miaka 11 la kucheza michezo 58 ya mashindano bila ya kushinda mchezo ama kutoka sare baada ya jana Jumamosi usiku kutoka sare ya bila kufungana na Visiwa vya Faroe kwenye mchezo wa kundi B wa kuwania kukata tiketi ya kufuzu fainali za kombe la dunia litakalofanyika mwakani nchini Urusi. 

    Ikicheza katika uwanja wake wa nyumbani wa Estadi Nacional,Andorra imeweza kupata pointi moja baada ya kuhimili kashikashi za wageni wao Visiwa vya Faroe waliokuwa pungufu baada ya nyota wake Joan Edmundsson kutolewa nje kwa kadi mbili za njano katika dakika ya 75 kwa mchezo mbaya.

    Mara ya mwisho Andorra yenye wakazi wapatao 80,000 kupata matokeo mazuri ya ushindi ama sare kwenye michezo yake ilikuwa ni mwaka 2005 pale ilipotoka sare ya 0-0 na Finland.

    Baada ya sare hiyo rekodi zinaonyesha kwamba Andorra imeshinda mchezo mmoja,imetoka sare mara tatu,imefungwa michezo 96.Imeruhusu wavu wake kuguswa mara 285.

    Akiongea baada ya mchezo huo kwisha nahodha wa Andorra,Ildefons Lima amesema "Tunafuraha kwa sababu tunajua sisi ni akina nani na jinsi gani imekuwa ngumu kwetu kuikabiri hali hii ya kupata matokeo mabaya.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Baada ya miaka 11 ya vichapo 58 hatimaye Andorra wapumua Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top