728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, March 29, 2017

    Msuva ataja siri ya Taifa Stars kushinda bila Mbwana Samatta


    Faridi Miraji.                                      

    Mshambuliaji wa timu ya Taifa Stars ( Tanzania),Simon Msuva ambaye kwenye mchezo wa Jana Jumanne aliweza kuifungia timu ya Taifa goli la kwanza kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi , amesema 

    " Si rahisi kushinda mchezo wowote bila kuwa na ushirikiano uwanjani na kila mchezaji kumpenda mchezaji mwenzake bila kujali aina ya timu anayochezea ( klabu ) maana kama tungecheza bila ushirikiano pasingetokea magoli yoyote ila nashukuru timu nzima Kocha wetu pia mashabiki wametufanya tuone sisi ni zaidi ya klabu zetu tunazozitumikia tukiwa kwenye ligi kuu au wale wanaocheza nje ya nchi " .


    " Ninachoweza kusema kuhusu Samatta ni kwer tulikuwa wapweke si kwa maana tusingeweza kucheza vzr ila wanaomjua Samatta ni zaidi ya kiongozi ni rafiki , mcheshi na pia anatia hamasa kubwa sana pindi tunapoingia uwanjani , ni kwer kwa uwezo wake na anahitajika kuwa na sisi kila mchezo ili atusaidie tunapokwama maana kama tunavojua mwenzetu kafika mbali kisoka na sisi tunahitaji kufika huko.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Msuva ataja siri ya Taifa Stars kushinda bila Mbwana Samatta Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top