728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, March 27, 2017

    Nini Mbwana Samatta , Sunday Manara " Computer " Mfungaji wa muda wote Taifa Stars


    Farid Miraji.
    Mashabiki wengi wa Tanzania wangependa kumfahamu mfungaji bora wa muda wote wa timu ya Taifa ya Tanzania.
    Kutokana na changamoto ya takwimu nchini itachukua muda kumaliza utata wa nani ndie hasa mfungaji bora wa muda wote japo kuna madai kuwa Sunday Manara anashikilia rekodi hio.
    Manara ambaye ni baba mzazi wa msemaji wa Simba, Haji Manara anatajwa kuifungia Taifa Stars mabao 28 katika mechi mbalimbali.
    Hakuna aliyethibitisha hilo kwa takwimu za uhakika zaidi ya fasihi simulizi za kupokezana bila utafiti wowote.
                                     
    Inawezekana ni kweli Manara mwenye umri wa miaka 61 alitimiza mabao hayo kwa kuwa miaka aliyocheza wachezaji walikuwa wana kawaida ya kudumu timu ya taifa kwa muda mrefu.
    Hata hivyo uchche wa mechi za kimataifa miaka hio ni sababu nyingine ya kutia shaka rekodi hio. Ukiondoa mechi za Kombe la Cecafa, timu ya Taifa ilikuwa ikicheza mechi chache sana za kimataifa miaka ya 1970-80 aliyocheza Manara.
    Kama ni kweli Manara alifunga mabao 28 basi mshambuliaji Mrisho Ngassa anahitaji mabao matatu zaidi kuifikia rekodi hio.
    Ngassa ameifungia Taifa Stars mabao 25 kati ya mwaka 2006 na 2013. Kwa sasa hajaichezea Taifa Stars tangu mwaka 2015 alipoitwa kwa mara ya mwisho wakati wa mechi dhidi ya Algeria jijini Dar.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Nini Mbwana Samatta , Sunday Manara " Computer " Mfungaji wa muda wote Taifa Stars Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top