728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, March 28, 2017

    Hatimaye Taifa Stars yafuta uteja kwa Burundi,yawagonga 2-1 U/Taifa


    Paul Manjale.
    Dar Es Salaam,Tanzania.

    HATIMAYE timu ya taifa ya Tanzania,Taifa Stars leo imefanikiwa kufuta uteja baada ya kuifunga timu ya taifa ya Burundi,Intamba M'urugamba mabao 2-1 katika mchezo mkali wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

    Simon Msuva ndiye aliyeanza kuipa uongozi wa mchezo Taifa Stars baada ya kufunga kwa shuti kali katika dakika ya 20 ya kipindi cha kwanza akiuwahi mpira wa kichwa wa Ibrahim Ajib ambao ulionekana kama upoteza uelekeo.Bao hilo lilidumu mpaka mapumziko.

    Kipindi cha pili Burundi walionekana kuimarika kimchezo na kufanikiwa kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake hatari,Laudit Mavugo katika dakika ya 53 ya mchezo.

    Mavugo alifunga bao hilo baada ya kuunasa mpira mrefu uliomshinda beki wa Taifa Stars,Abdi Banda na kumfunga kirahisi golikipa,Deogratius Munish "Dida' aliyekuwa ameliacha mbali kidogo lango lake.

    Mabadiliko ya kiufundi yaliyofanywa na kocha wa Taifa Stars,Salum Mayanga ya kumtoa Farid Mussa na kumuingiza,Mbaraka Yusuph Abeid yalizaa matunda baada ya mshambuliaji huyo wa Kagera Sugar kuifungia Taifa Stars bao la ushindi Katika dakika ya 77 ya mchezo.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Hatimaye Taifa Stars yafuta uteja kwa Burundi,yawagonga 2-1 U/Taifa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top