Barcelona,Hispania.
Barcelona wamewatolea macho Paulo Dybala na Antoine Griezmann kuimarisha kikosi chao majira ya kiangazi , kwa mujibu wa taarifa kutoka Mundo Deportivo.
Mabingwa hao wa La Liga wanahitaji mshambuliaji mwenye umri mdogo ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji , na nyota wa Juventus, Dybala na straika wa Atletico, Griezmann ndio wapo juu kwenye orodha yao na Barca wanatambua kwamba kila mchezaji gharama yake inafika Euro Milioni 100.
Kwa mujibu wa Mundo Deportivo, Dybala ameiarifu kambi yake kwamba anataka kuondoka Juventus na kuhamia Barcelona au Real Madrid.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina amesema kwamba hataki kuhamia Uingereza na anaamini kwamba ili kuboresha zaidi kiwango chake lazima ahamie Hispania.
0 comments:
Post a Comment