Peru.
ASKARI wanaoendesha vita ya kupambana na madawa haramu ya kulevya nchini Peru juzi Jumatano wamekamata madawa ya kulevya yenye uzito wa kilo 1,417 (Tani 1 na kilo 417) yakiwa na vifungio vyenye sura pamoja na nembo ya kibiashara ya staa wa Barcelona na Argentina,Lionel Messi.
Madawa hayo ambayo yamedaiwa kuwa yaliyokuwa yakisafirishwa kuelekea katika nchi za Ubelgiji na Marekani yameripotiwa kuwa na thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 85.
Madaiwa hayo yaliyokuwa yamefichwa ndani ya minofu ya samaki iliyokuwa imegandishwa kwa barafu pia yameripotiwa kuwa yaliyokuwa na vifungio vyenye nembo inayofanana na nembo ya Mfalme wa Hispania,Felipe VI.
Taarifa zaidi kutoka Peru zinasema mpaka sasa hakuna mtu yoyote aliyekamatwa ama kuripotiwa kutiwa nguvuni kwa kumiliki madawa hayo.
BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI http://www.stuff.co.nz/dominion-post/sport/football/90814454/
0 comments:
Post a Comment