Faridi Miraji
Mbio za ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania imefikia patamu huku mbio hizo zikitawaliwa na timu mbili za Simba na Yanga .
Simba ambayo imebakiza mechi sita ikiwa tatu kanda ya ziwa dhidi ya Kagera sugar ya Kagera, Mbao FC na Toto African zote za mwanza baada ya mechi za Kanda ya ziwa Simba watarudi Dar kumalizia mechi tatu dhidi ya African Lyon, Stand United na Mwadui Fc Huku wapinzani wao Yanga SC nao wamebakiza mechi sita kumaliza msimu wa ligi kuu mechi tano zitachezwa Dar dhidi ya Azam FC, Toto African, Kagera Sugar, Tanzania Prisons na Mbeya City , na moja dhidi ya Mbao Fc itachezwa Ccm Kirumba Mwanza. Katika mbio za ubingwa mpaka sasa Simba ndio vinara wakiongoza kwa pointi 55 akifuatiwa na Yanga yenye pointi 53
Kiungo wa Simba SC aliyepo kwa mkopo timu ya Mwadui Fc Awadhi Juma Maniche ameipa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom timu ya Simba SC Awadhi amesema ''Simba ina nafasi kubwa ya kubeba ubingwa wa ligi kuu kwa sababu wana morali nzuri kuliko Yanga''
Pia Awadhi Juma amepata kingungumizi kumtaja nani anaweza kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Awadhi amesema "Ni ngumu sana kumjua nani anaweza kuwa mfungaji bora kwa sababu bado mechi nyingi lolote linaweza kutokea ila nitafurahi akichukua mchezaji mzawa. Hasa Saimon Msuva au Ramadhan Kichuya."
Katika orodha ya ufungaji bora Saimon Msuva ndio anaongoza kwa ufungaji akiwa na magoli 12 akifuatiwa Kwa karibu na wazawa wawili Ramadhan Kichuya wa Simba Mwenye magoli 11 na Mbaraka Yusuph wa Kagera Sugar Mwenye magoli 10 .
Baadhi ya Wachezaji wa kimataifa Ambao Wapo kwenye mbio za kuwania kiatu hicho ni Amis Tambwe Mwenye magoli 9 Huku Donald Ngoma na Obrey Chirwa wakiwa na magoli 8 wachezaji wote Hawa wanaichezea Yanga SC.
0 comments:
Post a Comment