Paul Manjale.
Geneva,Uswisi.
SHIRIKISHO la soka duniani,FIFA limesema litamlipa mshahara kwa kipindi cha miezi sita beki wa Everton,Seamus Coleman ambaye Ijumaa iliyopita alivunjwa mguu wake wa kulia wakati akiichezea timu yake ya taifa ya Jamhuri ya Ireland kwenye mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya kombe la dunia dhidi ya timu ya taifa ya Wales huko kwenye uwanja wa Aviva,Jamhuri ya Ireland.
FIFA kupitia programu yake ya kinga kwa vilabu (Club Protection Programme) iliyoanzishwa Juni 2012 imekuwa na utamaduni wa kuvipunguzia mizigo vilabu kwa kuvisaidia kulipa mishahara na fidia wachezaji wanaopata majeraha mabaya wakati wanapokuwa wakizitumikia timu zao za taifa.
Coleman,28 alivunjika mfupa wa tibia Ijumaa iliyopita baada ya kuchezewa rafu mbaya na na beki wa Wales,Neil Taylor katika mchezo ulioisha kwa timu zao kutoka sare ya bila kufungana.
Hivyo FIFA kupitia programu yake ya kinga kwa vilabu itakuwa ikimlipa Coleman mshahara wa £50,000 kwa wiki katika kipindi chote atakachokuwa nje ya uwanja.Kiasi hicho ni kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa katika ya Coleman na Everton.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Jamhuri ya Ireland ,Coleman atakuwa nje ya uwanja mpaka mwaka 2018 baada ya Jumamosi iliyopita kufanyiwa upasuaji uliodaiwa kufanikiwa sana huko jijini Dublin.
0 comments:
Post a Comment