728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, March 31, 2017

    Antonio Valencia mchezaji bora wa mwezi Manchester United


    Manchester, England.

    BEKI wa kulia wa Manchester United,Antonio Valencia amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa klabu hiyo kwa mwezi wa tatu [Machi].

    Valencia,31,ambaye ni raia wa Ecuador ametwaa tuzo hiyo baada ya kujikusanyia asilimia 71 ya kura 80,000 zilizopigwa na mashabiki kupitia ukurasa rasmi wa Twitter wa klabu hiyo wa @ManUtd.

    Valencia atakumbukwa kwa kuonyesha kiwango bora kabisa katika michezo minne iliyopita ya Manchester Unuted kwa mwezi Machi dhidi ya FC Rostov,Bournemouth,Chelsea na kwenye mchezo dhidi ya Middlesbrough ambao alifunga bao lake la kwanza baada ya ukame wa miaka mitatu.Pia huo ulikuwa ni mchezo wake wa 200 akiwa na Manchester United.

    Nafasi ya pili imeenda kwa Marcos Rojo aliyepata asilimia 23 ya kura zote huku Ashley Young akishika nafasi ya tatu baada ya kujikusanyia asilimia 6 ya kura zote 80,000.

    Ikumbukwe kabla ya kutwaa tuzo ya mwezi wa Machi,tayari Valencia alikuwa ameshatwaa tuzo hiyo mara mbili katika miezi ya Novemba na Januari.Hivyo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyetwaa tuzo hiyo mara nyingi zaidi msimu huu klabuni Manchester United akifuatiwa na Zlatan Ibrahimovic aliyetwaa tuzo hiyo mara mbili katika miezi ya Disemba na Februari.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Antonio Valencia mchezaji bora wa mwezi Manchester United Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top