London,England
Kiungo wa Chelsea, N'Golo Kante ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi machi kwa kura zilizopigwa na mashabiki.
Kura 32,000 zilipigwa kupitia tovuti ya Sky Sports , huku Kante ambaye aliisaidia Chelsea kupata ushindi mara mbili mfululizo ugenini akijikusanyia kura 11,763 akiwapiku Romelu Lukaku na kiungo wa Spurs, Dele Alli.
Lukaku ambaye alifunga magoli 4 katika mechi 3 za mwezi machi amejikusanyia kura , 10,777 na Dele Alli aliyeshika nafasi ya tatu akipata kura , 4,069.
Straika wa Bournemouth, Josh King (3,114), Straika wa Leicester City, Jamie Vardy (1,290) na Winga wa Crystal Palace, Wilfried Zaha (1,251) . wakifunga idadi ya wachezaji 6.
0 comments:
Post a Comment