Paul Manjale,Dar Es Salaam.
LIGI kuu ya Vodacom Tanzania bara itaendelea tena leo Jumamosi kwa michezo minne kuchezwa, Stand United watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro Uwanja wa Kambarage,Shinyanga na Toto Africans wakiikaribisha Simba SC Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mechi nyingine za Jumamosi, Majimaji ya Songea itaifuata Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani -mchezo utakaoanza saa 8.00 mchana wakati JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Azam FC Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Kwa mujibu wa ratiba,Jumapili Mbao watacheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza huku Mwadui wakiwa wenyeji wa Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Mwadui,Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment