728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, April 24, 2017

    N'Golo Kante mchezaji bora ligi kuu England,Dele Alli, Bronze na waondoka na tabasamu.



    London,England.

    KIUNGO wa Chelsea,N'Golo Kante usiku wa kuamkia leo ameibuka kidedea baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa ligi kuu England kwa msimu wa 2016-17 katika hafla zilizofanyika kwenye hoteli ya Grosvenor,London.

    Kante,26,ametwaa tuzo hiyo baada ya kuonyesha soka akiwa na Chelsea aliyojiunga nayo Agosti mwaka jana kwa dau la £30m akitokea Leceister City.Kante amekuwa mchezaji wa kwanza kutoka Ufaransa kutwaa uchezaji bora tangu Thierry Henry afanye hivyo mwaka 2004.

    Wengine waliowania tuzo hiyo na kutoka mikono mitupu usiku wa jana ni Eden Hazard,Harry Kane,Romelu Lukaku, Zlatan Ibrahimovic na Alexis Sanchez.


    Tuzo ya mchezaji bora chipukizi imekwenda kwa mara ya pili mfululizo kwa kiungo wa Tottenham,Dele Alli.Tuzo ya mchezaji bora kwa wanawake imekwenda kwa staa wa Manchester City,Lucy Bronze ambaye pia ni mshindi wa mwaka 2014.


    Wengine walitwaa tuzo usiku wa jana ni pamoja na Jess Carter wa Birmingham City aliyetwaa tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwa upande wa wanawake.

    Nyota wa zamani wa Manchester United,DavidBeckham alipewa tuzo ya heshima  ya PFA's Merit award kutokana na kuwa na mchango mkubwa katika mchezo wa soka.






    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: N'Golo Kante mchezaji bora ligi kuu England,Dele Alli, Bronze na waondoka na tabasamu. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top