728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 21, 2017

    Barca yaendelea kuwekewa ngumu kumtumia Neymar El Clasico


    Barcelona,Hispania.

    MAJAALIWA ya Barcelona kutaka kumtumia Neymar kwenye mchezo wake wa wikendi hii wa ligi ya La Liga dhidi ya Real Madrid maarufu kama El Clasico yameendelea kupata upinzani mkali hii ni baada ya jana Alhamisi rufaa yao ya kupinga kufungiwa michezo mitatu kwa nyota huyo raia wa Brazil kutupiliwa mbali na kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka nchini Hispania,RFEF.

    Barcelona maarufu kama Blaugrana sasa italazimika kuipeleka rufaa hiyo mahakama ya usuluhishi ya masuala ya michezo (Court of Arbitration for Sport) leo Ijumaa na ikiwa itashinda, Neymar ataruhusiwa kuivaa Real Madrid siku ya Jumapili huko dimbani Santiago Bernabeu.


    Mapema mwezi huu Neymar alitolewa uwanjani kwa kadi mbili za njano kwa utovu wa nidhamu kwenye mchezo ambao Barcelona ilichapwa mabao 2-0 na Malaga huko La Rosaleda ambapo adhabu yake ilikuwa ni kukosa mchezo mmoja.

    Taarifa iliyotolewa baadae na Kamisaa wa mchezo huo,Jesus Gil Manzano ilimbana zaidi Neymar baada ya kuonyesha kuwa staa huyo wa zamani wa Santos alimpigia makofi ya kejeli mwamuzi msaidizi wakati anatoka uwanjani na kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.Tukio hilo liliambatana na adhabu ya kukosa michezo miwili.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Barca yaendelea kuwekewa ngumu kumtumia Neymar El Clasico Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top