728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, April 22, 2017

    Hii hapa tano bora ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka Mwafrika ligi kuu Ubelgiji


    Genk,Ubelgiji.

    LICHA ya kuiongoza klabu yake ya KRC Genk kufika robo fainali ya michuano ya Europa Ligi,Mtanzania Mbwana Ally Samatta ameshindwa kuingia tano bora ya wachezaji wanaowania tuzo ya Ebony Shoe Award.

    Tuzo hiyo ambayo inaingia katika msimu wake wa 25 hutolewa maalumu kuwapongeza wachezaji wa Afrika au wenye asili ya Afrika ambao wamefanya vizuri kwenye ligi kuu ya soka ya nchini Ubelgiji.

    Wachezaji waliopenya tano bora msimu huu ni pamoja na mshambuliaji hatari wa KAS Eupen,Mnigeria Henry Onyekuru aliyefunga mabao 18 mpaka sasa.Mabao 14 yakiwa ni ya ligi kuu Ubelgiji,manne ya michuano mingine.

    420_0900_24547_20170401_hagemann_0731.jpg

    Henry Onyekuru

    Wengine ni Mbaye Leye wa Zulte Waregem na Senegal, Mshindi wa tuzo hiyo kwa msimu uliopita Sofiane Hanni wa Anderlecht na Algeria.Landry Dimata wa KV Oostende na Congo DR na Youri Tielemans wa Anderlecht na Ubelgiji/Congo DR.

    Baadhi ya nyota waliowahi kutwaa tuzo hiyo ni pamoja na Vincent Kompany,Daniel Amokachi, Celestine Babayaro,Romelu Lukaku,Marouane Fellaini,Victor Ikpeba,Godwin Okpara na Michy Batshuayi.

    Tuzo hiyo ilianza kutolewa mwaka 1992 na mshindi wake wa kwanza alikuwa ni Mnigeria,Daniel Amokachi.Congo DR ndiyo taifa linaloongoza kutwa tuzo hiyo mara nyingi zaidi.Jumla limetwaa tuzo hiyo mara nane.

    Mbark Boussoufa wa Morocco ndiye mchezaji anayeongoza kutwaa tuzo hiyo mara nyingi zaidi.Ametwaa tuzo hiyo mara tatu (3) akifuatiwa na Daniel Amokachi na Vincent
    Kompany waliotwaa tuzo hiyo mara mbili kila mmoja.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Hii hapa tano bora ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka Mwafrika ligi kuu Ubelgiji Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top