London, England.
STAA wa zamani wa Nigeria,Austin ‘Jay-Jay’ Okocha amemuonya staa wa Arsenal ambaye pia ni mpwa wake,Alex Iwobi kutofikiria kuihama klabu hiyo kwa uhamisho wa mkopo katika dirisha lijalo la usajili barani Ulaya kwani kufanya hivyo kutamharibia.
Okocha ametoa onyo hilo baada ya hivi karibuni Iwobi,20,kujikuta akisugua benchi mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza cha Mfaransa,Arsene Wenger kutokana na kushindwa vita ya kugombea namba.
Okocha aliyewahi kutamba vilivyo na klabu ya Bolton Wanderers kabla ya kuamua kutundika daruga ameiambia Sky Sports kuwa Iwobi hapaswi kuhama na badala yake anapaswa kubaki na kupambana ili aweze kurejea tena kikosi cha kwanza.
Nafikiri ni vyema akabaki Arsenal kwa sababu aina yake ya uchezaji inaendana sana na soka linalochezwa na klabu hiyo.Akienda kwingine atapata wakati mgumu kuzoea.Anapaswa kubaki na kupigania jezi yake Arsenal.
0 comments:
Post a Comment