Barcelona,Hispania.
LUIS Suarez na Ivan Rakitic wameendelea kuiweka Barcelona kileleni mwa msimamo wa ligi ya La Liga baada ya usiku wa leo kuifungia miamba hiyo matatu katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wapinzani wao wa jimbo la Catalunya,Espanyol.
Suarez alianza kuipa uongozi Barcelona baada ya kuifungia bao la kwanza katika dakika ya 50.Dakika ya 76 Rakitic alifunga bao la pili kabla ya Suarez kuongeza la tatu katika dakika ya 87.
Ushindi huo umeifanya Barcelona ifikishe pointi 81 sawa na wapinzani wao Real Madrid wenye mchezo mmoja mkononi.Barcelona wamecheza michezo 34 huku Real Madrid wakicheza michezo 33.
0 comments:
Post a Comment