Turin,Italia.
JUVENTUS imefanikiwa kumsajili kiungo wa kimataifa wa Uruguay,Rodrigo Bentancur maarufu kama 'Lolo' kutoka klabu ya Boca Juniors ya Argentina kwa ada ya £8m.
Bentancur mwenye umri wa mika 19 ameingia kandarasi ya miaka mitano ya kuitumikia miamba hiyo ya jiji la Turin na Julai 1 mwaka huu atatangazwa rasmi kuwa mchezaji wake mpya.
Juventus imemnasa Bentancur ambaye pia alikuwa akiwindwa na vilabu vya Manchester United na Arsenal baada ya Juni 2015 kumhusisha katika mauzo ya mshambuliaji Carlos Tevez aliyekuwa anaihama miamba hiyo ya Italia na kurejea nyumbani Boca Juniors.
Wakati huohuo habari zinasema kuwa Boca Juniors itapata mgao wa asilimia hamsini (50%) kutoka katika mauzo yoyote yale yatakayomuhusisha kiungo huyo anayeichezea pia timu ya vijana ya Uruguay ya U20.
Bentancur alijiunga na Boca Juniors akiwa na umri wa miaka 14 na Aprili 2015 akiwa na umri wa miaka 17 alipata bahati ya kucheza mchezo wake wa kwanza akiwa na kikosi cha wakubwa cha klabu hiyo ya La Bombonera.
0 comments:
Post a Comment