London,England.
BAADA ya wiki iliyopita nyota wa zamani wa Nigeria, Austin Jay Jay Okocha kudai kuwa mpwa wake,Alex Iwobi anapigwa benchi klabuni Arsenal kutokana na kurejea kwa wachezaji waandamizi waliokuwa majeruhi,kocha wa klabu hiyo Mfaransa Arsene Wenger amepinga madai hayo na kutoa ufafanuzi wa kile kinachomweka benchi kinda huyo mwenye umri wa miaka 20.
Wenger amesema kukosekana kwa Iwobi katika michezo mitatu iliyopita ya ligi kuu England kunatokana na kubadilika kwa mfumo wa uchezaji klabuni hapo ambao umewafanya wachezaji kama Theo Walcott na wengine wengi wajikute wakiwa nje ya kikosi cha kwanza.
Kwa sasa Arsenal inatumia mfumo mpya wa 3-5-2 kutoka ule wa zamani wa 4-2-3-1.
Wakati huohuo Wenger amesema kuwa Arsenal itakuwa ikibadili mfumo kulingana na aina ya mpinzani watakayekutana nae kabla ya kufika mwisho kwa msimu huu wa ligi kuu England hivyo bado kuna nafasi kwa Iwobi kurejea kikosini.
0 comments:
Post a Comment