728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 28, 2017

    Nabil Maaloul Kocha Mpya Tunisia


    Tunis,Tunisia.

    TUNISIA imemteua mzawa, Nabil Maaloul kuwa kocha mkuu mpya wa timu yake ya taifa.

    Maaloul mwenye umri wa miaka 54 na kocha wa zamani wa Espérance Sportive de Tunis na El-Jaish SC ya Qatari anachukua mikoba ya Mpolandi,Henryk Kasperczak aliyefutwa kazi wiki kadhaa zilizopita 

    Kasperczak alifutwa kazi baada ya Tunisia kushindwa kutamba kwenye fainali zilizopita za michuano ya AFCON iliyofanyika nchini Gabon na Cameroon kuibuka mabingwa.

    Maaloul anarejea kuifundisha Tunisia kwa mara ya pili.Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2013 ambapo alihudumu kwa miezi saba pekee kabla ya kutimkia Kuwaiti ambapo alipewa kibarua cha kuifundisha timu ya taifa ya nchi hiyo.

    Jukumu kubwa alilopewa Maaloul ni kuhakikisha Tunisia inafuzu michuano ya AFCON ya mwaka 2019 ambapo imepanga kundi J pamoja na mataifa ya Misri,Niger na Swaziland.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Nabil Maaloul Kocha Mpya Tunisia Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top