728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 20, 2017

    Wakisaini hawa ukata basi Jangwani


      
    Farid Miraji,Dar Es Salaam.

    Timu ya  Yanga SC ambayo Kwa sasa haipo vizuri kifedha baada ya mwenyekiti Wao ambaye alikuwa mfadhili kupata matatizo na kutokuwa karibu na timu mpaka kupelekea baadhi ya wachezaji kugoma kutokana na mishahara yao kuchelewa kupewa. Iwapo tu mpango huu ukitiki na kusainishana mikataba ukata YANGA utakoma Mara moja . kampuni kutoka KENYA ya SportsPesa wanatarajia kuingia mkataba wa miaka mitano na Yanga wenye thamani ya Billion 4.5 Kwa miaka Mitano  ambao kwa mwaka utakuwa na thamani ya Sh milioni 900. 

    Uongozi wa Yanga leo utakutana na wawakilishi wa kampuni hiyo, ambapo wakikubaliana wataingia mkataba huo wa miaka mitano ambao kila mwaka utakuwa na nyongeza ya asilimia sita ya fedha. Asilimia sita ya milioni 900 ni milioni 54 Kwa hiyo Yanga watakuwa wanaongezewa million 54 Kwa miaka minne yanga wanaongezewa milioni 216 Kwa mkataba wao Kwa miaka Mitano pamoja na nyongeza ya asilimia sita Itakuwa ni Jumla ya Billion 4.716 Kwa miaka yote Mitano. 

    "leo wawakilishi wa SportPesa watakutana na uongozi wa Yanga ili kumalizana nao juu ya mkataba wanaotaka kuingia na hiyo ni kutokana na kufika makubaliano ya kimkataba," Alisema mjumbe wa kamati kuu ya Yanga 

    Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, ambaye alisema wapo kwenye hatua za mwisho za kuingia mkataba na SportsPesa.

    "Napenda nizungumze kitu kilichokua tayari au kimekamilika hatua ya kuingia mkataba na SportsPesa bado, ila tutakutana nao kwa mazungumzo ya mwisho ambayo yatatoa jibu kama watatudhamini au la.

    "Tunazungumza na SportsPesa kwa kuwa hawa wamekuja moja kwa moja kwetu tofauti na kampuni nyingine ambazo zinataka kutudhamini, lakini ipo kampuni tuliyoipa jukumu la kufanya mazungumzo nao nasi kutuletea taarifa ya kila kinachoendelea." alisema Mkwasa.

    Iwapo Yanga watamalizana na kampuni SportsPesa ya Kenya Itakuwa timu ambayo inalipwa vizuri Africa Mashariki . Kwa Tanzania mikataba ya awali waliyosaini Simba na Yanga kwa Kilimanjaro walikuwa wanapewa milioni 500 Kwa mwaka ila Azam Fc wanapata Bilioni 1 Kwa mwaka kama udhamini kupitia Nmb na Azam Cola kwenye mkataba wa Azam na Nmb kila mwaka Nmb hutoa Milioni 600 kwa Azam Ingawa ni Siri Sana Huku Azam cola ambao mwanzoni walikuwa wadhamini wakuu wanatoa Milioni 400 Kwa Mwaka ,  timu nyingine Ambayo inaudhamini mzuri ni timu ya Mbeya City ikidhaminiwa na RB Bettery Kutoka Bin Slum na Coca-Cola  inakadiliwa Mbeya City Wanapokea Milioni 400 Kwa Mwaka Kwa Mikataba ya RB na Coca-Cola. 


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Wakisaini hawa ukata basi Jangwani Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top