Munich,Ujerumani.
Borussia Dortmund sasa itakutana na Eintracht Frankfurt kwenye mchezo wa fainali wa kuwania kombe la Ujerumani maarufu kama DFB Pokal baada ya usiku huu kuifunga Bayern Munich mabao 3-2 kwenye mchezo wa nusu fainali uliochezwa dimbani Allianz Arena.
Marco Reus aliipa uongozi Borussia Dortmund baada ya kuifungia bao la kwanza katika dakika ya 19 akitumia vyema makosa ya Javi
Martinez aliyerudisha mpira nyuma bila kuangalia na kumkuta mfungaji.
Dakika ya 28 Javi Martinez alisawazisha makosa yake na kuifungia Bayern Munich bao la kusawazisha kabla ya Mats Hummels kuongeza bao la pili katika dakika ya 41 na kufanya mchezo uende mapumziko matokeo yakiwa 2-1.
Kipindi cha pili kilikuwa kizuri zaidi kwa Borussia Dortmund kwani waliweza kuwabana vyema wenyeji wao Bayern Munich na kufanikiwa kupata mabao mawili ya dakika za 69 na 74 kupitia kwa Pierre-Emerick Aubameyang na Ousmane Dembele.
Katika mchezo mwingine wa nusu fainali Eintracht Frankfurt ambao wanashika nafasi ya tisa Bundesliga wamefanikiwa kutinga fainali baada ya kuifunga Borussia Monchengladbach kwa penati 7-6.Mchezo wa fainali utafanyika Mei 27 huko Berlin kwenye dimba la Olympiastadion .
0 comments:
Post a Comment