Genk,Ubelgiji.
KLABU ya KRC Genk inayochezewa na Mtanzania, Mbwana Samatta imeendelea kujiweka katika mazingira mazuri ya kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Europa Ligi kwa mara ya pili mfululizo baada ya usiku wa kuamkia leo kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya KV Kortrijk katika mchezo wa kundi A wa hatua ya mtoano uliochezwa huko Luminus Arena.
Katika mchezo huo ambao Samataa alianzia benchi kabla ya kuingia katika dakika ya 66 ilishuhudiwa Genk ikijipatia mabao yake kupitia kwa Leandro Trossard aliyefungwa kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 14 na Siebe Schrijvers aliyefunga mabao mawili katika dakika za 45 na 70 akitumia vyema pasi ya Leandro Trossard na mpira wa Samatta uliogonga mwamba na kurejea uwanjani.
Ushindi huo umeifanya KRC Genk ifikishe pointi 16 baada ya kushuka dimbani mara 6 na kuongoza kundi B.Lokeren ni ya pili ikiwa na pointi 9 huku KV Kortrijk ikiwa ya tatu na pointi 6.
0 comments:
Post a Comment