Madrid,Hispania.
CRISTIANO Ronaldo (Pichani) amefunga mabao matatu (hat trick) na kuiwezesha Real Madrid kuifunga Bayern Munich mabao 4-2 katika mchezo wa marudiano wa hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe na klabu bingwa Ulaya uliochezwa huko Santiago Bernabeu,Madrid.
Katika mchezo huo uliolazimika kuchezwa kwa dakika 120 baada ya Bayern Munich kuwa mbele kwa mabao 2-1 katika tisini za kawaida ilishuhudiwa Ronaldo,32,akifunga mabao yake matatu katika dakika za 76', 105' na 110 na kuwa mchezaji wa kwanza kufikisha mabao 100 kwenye michuano hiyo.Bao la nne la Real Madrid limefungwa na kinda,Marco Asensio katika dakika ya 112 na kuipeleka miamba hiyo nusu fainali kwa mara ya saba mfululizo.
Mabao ya Bayern Munich iliyolazimika kumaliza mchezo ikiwa pungufu baada ya Arturo Vidal kutolewa nje kwa kadi mbili za njano na mwamuzi Victor Kassai kutoka Hungary katika dakika ya 84 yamefungwa na Robert Lewandowski kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 53 pamoja na bao la kujifunga la Sergio Ramos katika dakika ya 77.
Ushindi huo umeifanya Real Madrid iwe imeing'oa Bayern Munich kwa ushindi wa jumla wa mabao 6-2.Ikumbukwe katika mchezo wa awali uliochezwa jijini Munich Jumanne iliyopita Real Madrid ilishinda mabao 2-1.
Droo ya upangaji wa ratiba ya nusu fainali itafanyika kesho kutwa Ijumaa.
Vikosi
Real Madrid: Navas; Carvajal, Ramos,Nacho, Marcelo; Casemiro, Kroos (Kovacic), Modric; Isco (Vazquez),Benzema (Asensio), Ronaldo.
Bayern Munich: Neuer; Lahm, Boateng,Hummels, Alaba; Alonso (Muller), Vidal, Thiago; Robben, Ribery (Douglas Costa),Lewandowski (Kimmich).
0 comments:
Post a Comment