Genk,Ubelgiji.
MBWANA Samatta ameshindwa kuweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano ya Europa Ligi baada ya usiku wa kuamkia leo klabu yake ya Genk ya Ubelgiji kutupwa nje ya michuano hiyo kufuatia kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Celta Vigo ya Hispania kwenye mchezo wa robo fainali ya pili uliochezwa huko Luminus Arena,Genk.
Licha ya wenyeji Genk kutawala mchezo kwa kiwango kikubwa lakini walikuwa ni wageni Celta Vigo ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao baada ya Pione Sisto kufunga katika dakika ya 63.Bao hilo halikudumu sana kwani katika dakika ya 67 Leandro Trossard aliifungia Genk bao la kusawazisha na kufanya mchezo uishe kwa sare ya bao 1-1.
Kwa sare hiyo sasa Celta Vigo inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3.Ikumbukwe katika mchezo wa awali uliochezwa huko Balaidos,miamba hiyo ya Hispania ilitoka nyuma na kuifunga Genk mabao 3-2.
Genk iliwakilishwa na:Matthew Ryan,Timoty Castagne,Jakub Brabec,Omar Colley Jere Uronen,Sander Berge,Alejandro Pozuelo,Ruslan Malinovsky,Leandro Trossard,Mbwana Samatta na Thomas Buffel
0 comments:
Post a Comment