728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, April 23, 2017

    Zimerudi:Simba SC yapokwa pointi tatu za Kagera Sugar



    Dar Es Salaam,Tanzania.

    Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF imefikia maamuzi ya Kutengua Maamuzi ya Kamati ya Saa 72 iliyowapa Simba SC pointi tatu na magoli matatu kwa madai kwamba Kagera Sugar kwenye ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Simba katika mechi ya Ligi kuu iliyochezwa Aprili 2 Mwaka huu Uwanja wa Kaitaba, walimchezesha Mlinzi Mohamed Fakhi Gharib aliyedaiwa kuwa na kadi tatu za njano.

    Katibu mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa amethibitisha kagera Sugar kurudishia pointi tatu walizopokwa.

    "Kikao cha Kamati maarufu ya saa 72 Kilikosa uhalali baada ya kuwashirikisha wajumbe waalikwa ambao sio sehemu ya kamati hiyo

    Matokeo ya Kagera Sugar na Simba yanabaki kama yalivyokuwa awali. (Kagera Sugar 2-1 Simba SC.

    Vilevile kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji imemuagiza Katibu mkuu wa TFF kuwapelekea katika kamati za kinidhamu na Maadili baadhi ya Watendaji wa bodi ya Ligi kwa kutowajibika na kuipotosha kamati ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi". Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, Celestine Mwesigwa amewaambia Waandishi wa Habari Jioni ya leo.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Zimerudi:Simba SC yapokwa pointi tatu za Kagera Sugar Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top