728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, April 30, 2017

    Spurs yatumia sekunde 146 kuimaliza Arsenal ligi kuu England


    London,England.

    TOTTENHAM imewatoa nishai wapinzani wao wa jadi wa kaskazini mwa jiji la London,Arsenal baada ya kuwaadhibu kwa kuwachapa mabao 2-0 katika mchezo mkali wa ligi kuu England ulioisha hivi punde katika dimba la White Hart Lane.



    Tottenham imejipatia mabao yote katika kipindi cha pili cha mchezo kupitia kwa Dele Alli dakika ya 57 na Harry Kane dakika ya 58 aliyefunga kwa mkwaju wa penati uliopatikana baada ya yeye mwenyewe kuangushwa ndani ya boksi na beki wa Arsenal,Gabriel Paulista.


    Ushindi huo umeipa Tottenham upenyo wa kumaliza ligi juu ya Arsenal kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1995 hii ni kwa sababu imefikisha pointi 77.Pointi 17 mbele ya wapinzani wao hao wenye pointi 60.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Spurs yatumia sekunde 146 kuimaliza Arsenal ligi kuu England Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top