Dodoma,Tanzania.
MABINGWA watetezi wa ligi kuu na mabingwa wa kombe la FA,Yanga SC leo jioni watashuka kwenye dimba la Jamhuri mkoani Dodoma kucheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya timu ya Kombaini ya Majeshi ya Tanzania.
Mchezo huo utakaokuwa maalumu kwa ajili ya kusherekea miaka 53 ya uhai wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake mishale ya saa 10:00 jioni.
Yanga SC ambayo tayari iko mkoani Dodoma tangu jana Jumanne inatarajiwa kuutumia mchezo wa leo kujiwinda na mchezo wake wa kombe la FA utakaochezwa wikendi hii dhidi ya Mbao FC huko CCM Kirumba jijini Mwanza.
0 comments:
Post a Comment