Liverpool, England.
LIVERPOOL imeangukia pua baada ya usiku huu ikiwa nyumbani Anfield kufungwa mabao 2-1 na Crystal Palace katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu England.
Liverpool ndiyo waliokuwa wa kwanza kuandika bao baada ya kiungo wake Philippe Coutinho kufunga bao safi kwa mkwaju wa faulo.
Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha Crystal Palace ambao walikuja juu na kufanikiwa kupata mabao mawili kupitia kwa mshambuliani wake wa kimataifa wa Ubelgiji,Christian Benteke.
Ushindi huo umeifanya Crystal Palace kujinasua kutoka na kukaa pointi saba juu ya mstali wa kushuka daraja.
0 comments:
Post a Comment