728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 19, 2017

    Suala la Fakhi ni unafki wa TFF na kamati zao


    Yossima Sitta Jr .  Dar es salaam                                             

    Suala la sakata la kadi tatu za njano za Fakhi linaendelea kuibua Madudu ya Tff na kamati zao haiwezekani suala kama hili la kikanuni kinaanza kupelekwa kisiasa Sijawahi ona haya maajabu ya Soka ni Hapa Tanzania tu.  Raisi wa Tff Kwa hili na yanayoendelea kuhusu utata wa maamuzi ya kadi tatu za Fakhi Huna budi hata ujiuzulu Kabsa ili kulinda heshima Yako hata kidogo. 

    Kagera sugar iliifunga Simba uwanjani Kwa magoli mawili Kwa moja Simba wakakata rufaa Bodi ya ligi kuhusu Kagera sugar kumchezesha Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano pia wakaenda mbali zaidi wakataja mechi alizopata kadi na dakika aliyopewa kadi hili ni tatizo kwenye management za TFF kama ni kiongozi nani aliyewapa data hizi Simba?  Sina tatizo na Simba kukata rufaa maana ni haki yao kikatiba. 

    Baadae kamati ya masaa 72 ulikaa na kupitia ripoti za waamuzi na Kuwaita Mwamuzi wa mchezo na kamisaa wa mchezo huo baada ya kikao Kamati ya masaa 72 walijiridhisha Kagera sugar wamemtumia Fakhi akiwa na kadi tatu za njano wakaipa Simba pointi tatu na magoli matatu baadae hata siku haijaisha Kagera Sugar kupitia Kwa mwenyekiti Wao wakaandika Barua kwenda Kwa Katibu mkuu wa TFF wakiomba marejeo (review)  ya hukumu yao Huku wakipinga vikali kupokwa pointi tatu na kamati ya masaa 72 na kupewa Simba.  Katibu wa Tff akaitisha kikao cha kamati nyingine kamati ya katiba, Sheria na hadhi za wachezaji kufanya marejeo ya barua yao ila Katibu akaenda mbali zaidi na Kuwaita wahusika wengi kuja kutoa ushahidi mojawapo walioitwaa ni viongoz wa kagera sugar,  Marefa wote wa mchezo wa Kagera sugar na African Lyon,  viongozi wa African Lyon,  viongozi wa Simba pamoja na Viongoz kutoka Bodi ya ligi ambao ndio watunza data na ripoti za michezo ya ligi kuu. 

    Baada Simba kupewa pointi 3 za mechi ya Kagera, sasa soka linaingia kwenye siasa za hovyo. Kila mmoja anaongea lake kamati zinapingana zenyewe Kwa zenyewe. Kama Hujui Kila mechi ripoti zake hujazwa kwa maandishi na kutumwa Bodi ya ligi kabla ya masaa 48. Ripoti hizo ndizo hupaswa kupitiwa na uamuzi kufanywa pale rufaa inapokatwa kweli Leo tumeshidwa kuziamini mpaka tuanzee Kuwaita watu ambao hata hawahusiki? Unamuitaje mtu kutoa ushahidi kuhusu timu yake atakubali?  Leo viongozi wa Simba watakubali Fakhi hana kadi tatu za njano?  Au viongoz wa kagera au Fakhi Mwenye atakubali kosa?  Yaani tunashidwa kuamini kilichoandikwa Kwa mandishi tunataka kuamini vichwa vya watu ambao tena wana maslahi na Jambo lenyewe.  

    Malinzi na viongozi wako mnakolipeleka Soka la Tanzania si mahali sahihi siasa za usimba na uyanga mnazoziingiza kwenye kamati za maamuzi siku moja yatatutokea puani huwezi kupindisha pindisha ishuu dogo kama Hii.  Na Hii sarakasi ya maamuzi kuhusu Jambo hili ni unafiki wa tff na viongoz wake. Naanza kukumbuka ya nyuma hadi kichwa kinauma suala la Hassan Kessy kusajiliwa Yanga ilibainika kuna afisa mmoja ndani ya Tff aliwandanganya Yanga Kessy amemaliza mkataba na Simba Jina lake likatumwa CAF,  issue ya Ludovic Venance hili nalo tuakaambiwa kuna afisa mmoja alimpa Leseni Ludovic kimakosa.  Haya yote ni kufeli Kwa kamati zako na Viongoz waliopo chini Yako. 

    Jana usiku niliandika Andishi kuhusu kinachoenda kuzungumzwa na Simba leo sa 5:30 na viongozi wa Simba kuhusu sakata la Fakhi Andishi lilikuwa na kichwa kinachosema  (SAKATA LA FAKHI HALI TETE MSIMBAZI) Niliamua kulifuta Kwa maslai ya mkutano huo  yaani imekuwa kutishiana tu kwa sasa watakayoenda kuzungumza Simba ndio ambayo waliongea Yanga hapo nyuma baada ya kamati ya masaa 72 kuipa Simba pointi tatu.  Kama Soka letu tutaliendesha hivi ipo siku watu wataacha kuupenda Mpira wa miguu wa Tanzania Siasa za usimba na uyanga utaua Soka letu.  


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Suala la Fakhi ni unafki wa TFF na kamati zao Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top