Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka kumi na saba Serengeti Boys wameshinda tena mchezo wa marudiano wa kirafiki dhidi ya Gabon na kupata ushindi wa magoli mawili kwa moja.
Wafungaji Kwa upande wa Tanzania (u17) Serengeti boys ni Assad Juma Ally dakika ya 31 na Abdul Hamis Suleiman dakika ya 41 .
-Hii ilikuwa mechi ya marudiano baada ya Ile ya awali iliyochezwa jumamosi na Serengetiboys kushida Kwa mabao mawili Kwa moja (2-1) Gabon ndio mwenyeji wa AFCON chini ya miaka kumi na Saba mwaka huu.
Serengeti boys baada ya mechi ya leo itaenda Cameroon kucheza mechi za kirafiki na timu ya Cameroon (U17). Mechi dhidi ya Cameroon Itakuwa ya mwisho Kwa Serengetiboys kabla ya kwenda Gabon .
Makundi AFCON (U17) 2017
Kundi A
-Gabon
-Cameroon
-Ghana
-Guinea
Kundi B
-Tanzania
-Angola
-Niger
-Ethiopia
0 comments:
Post a Comment