Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya waamuzi watakaochezesha Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 nchini Gabon baadaye mwezi ujao.
Mwamuzi msaidizi wa Tanzania, Frank Komba ni kati ya jumla ya waamuzi 29 wa kati na pembeni walioteuliwa katika mashindano hayo yanayotarajiwa kupamba moto kati ya Mwi 14-28.
Ikumbukwe CAF) haikuteua mwamuzi hata mmoja kutoka Tanzania kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 nchini Zambia mwezi uliopita.
0 comments:
Post a Comment