728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 21, 2017

    Rashford aipeleka Man United nusu fainali Europa Ligi, Depay na Lyon yake nao wapenya


    Manchester,England.

    KWA MARA nyingine tena mshambuliaji kinda wa England,Marcus Rashford (Pichani) ameibuka shujaa baada ya Alhamis usiku kuifungia klabu yake ya Manchester United bao la ushindi la dakika ya 107 katika ushindi wa mabao 2-1dhidi ya Anderlecht katika mchezo wa wa pili wa hatua ya robo fainali uliochezwa dimbani Old Trafford.

    Katika mchezo huo uliolazimika kuchezwa kwa dakika 120 ili kumpata mshindi ilishuhudiwa Henrikh Mkhitaryan akiifungia Manchester United bao la kuongoza katika dakika ya 10 kabla ya nahodha Sofiane Hanni kuifungia Anderlecht bao la kusawazisha katika dakika ya 37 na kufanya dakika tisini (90) za mchezo huo ziishe matokeo yakiwa sare ya bao 1-1. 

    Ushindi huo umeifanya Manchester United ifuzu nusu fainali na kuwa moja kati ya timu nne zinazowania kucheza fainali ya michuano hiyo itakayofanyika Mei 24 huko Stockholm,Sweden.

    Katika mchezo mwingine Olympique Lyon ya Ufaransa inayochezewa na winga wa zamani wa Manchester United Mdachi,Memphis Depay nayo imefuzu nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuiondosha Besktasi ya Uturuki kwa mikwaju 7-6 ya penati baada ya sare ya mabao 3-3.

    Mbali ya Manchester United na Olympique Lyon vilabu vingine ambavyo vimefuzu nusu fainali na Ajax ya Uholanzi na Celta Vigo ya Hispania.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Rashford aipeleka Man United nusu fainali Europa Ligi, Depay na Lyon yake nao wapenya Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top