London, England.
VILABU vya Chelsea na Tottenham Hotspur vimeendelea kuonyesha umwamba wao kwenye ligi kuu ya soka nchini England baada ya kutoa wachezaji wanne wanne kila kimoja kwenye kikosi bora cha mwaka cha ligi hiyo maarufu kama PFA Premier League Team of the Year.
Katika kikosi hicho kilichotangazwa leo asubuhi vilabu vya Manchester United,Liverpool na Everton vimetoa mchezaji mmoja mmoja huku Arsenal na Manchester City zikishindwa kutoa mwakilishi hata mmoja katika kikosi hicho ambacho huchaguliwa kwa kupigiwa kura na wachezaji wa kulipwa.
Zlatan Ibrahimovic na Alexis Sanchez ambao ni kati ya wachezaji watano wanaowania tuzo ya kumsaka mchezaji bora wa mwaka wao wameshindwa kupenya kabisa kwenye kikosi hicho ambacho kitatambulishwa rasmi Jumapili Aprili 23 kwenye hafla itakayofanyika kwenye hoteli ya Grosvenor House iliyoko jijini London.
Hafla hiyo pia itatumika kuwazawadia wachezaji waliofanya vizuri kwenye ligi kuu kwa msimu wa 2016/17 ambapo tuzo za mchezaji bora wa kike na wa kiume zitatolewa pamoja na tuzo za kocha bora wa mwaka.
Kikosi Kamili
Kipa: David de Gea (Manchester United)
Mabeki:Kyle Walker (Tottenham Hotspur),David Luiz (Chelsea), Gary Cahill (Chelsea),Danny Rose (Tottenham Hotspur)
Viungo: Dele Alli (Tottenham Hotspur),Eden Hazard (Chelsea), N'Golo Kanté (Chelsea), Sadio Mane (Liverpool)
Washambuliaji:Harry Kane (Tottenham Hotspur),Romelu Lukaku (Everton)
0 comments:
Post a Comment