Farid Miraji,Dar Es Salaam.
Mshambuliaji ghali Hapa nchini Obrey Chirwa mambo yake si mazuri ndani ya Yanga muda wowote siku yoyote mkataba wake utavunjwa . Habari kutoka ndani ya uongozi wa Yanga umepanga kuachana na Mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia Kwa sababu ambazo hazitajwi. Lakini chanzo chetu kutoka ndani ya Yanga kinasema viongozi wamedhamilia kuachana na Chirwa Kwa sababu kuu mbili moja mshahara wake Mkubwa ambao Yanga wameshidwa kuulipa kingine ni mgomo alioufanya hivi karibuni .
Mshambuliaji huyo aligoma kuungana na timu iliyoenda Algeria kucheza mechi ya marudiano ya kombe la shirikisho dhidi ya MC Alger akidai anawadai Yanga malimbikizo ya mishahara ya miezi mitatu . Katika mchezo huo yanga Walienda kufungwa Kwa mabao manne Kwa bila (4-0) na kutolewa Kwa Jumla ya mabao manne Kwa moja (4-1).
Chirwa aliyesajiliwa na Yanga kutoka Platinum Fc ya Zimbambwe Kwa dau la zaidi ya milioni 200 za Kitanzania na kusaini mkataba wa miaka miwili anaolipwa zaidi ya milion kumi Kwa mwezi Mkataba wake utaisha mwezi wa kwanza mwakani (January 2018). Wakati Yanga wakipanga kuvunja mkataba wa Chirwa Mshambuliaji huyo Leo(jana) ameomba msamaha na kuungana na wachezaji wenzake Katika uwanja wa Polisi kilwa Road kwa mazoezi ya kujiandaa na mechi ya kombe la Shirikisho (ASFC) utakaochezwa jumamosi ya April 22 uwanja wa taifa.
Yanga ambayo inawachezaji saba wa kimataifa wengi Wao mikataba yao inaelekea Kiisha mwisho wa msimu wachezaji wa kimataifa ambao mikataba yao inaisha mwisho wa msimu ni beki wa Togo Vicente Bossue, Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi Amis Tambwe, Wazimbambwe wawili Donald Ngoma na Thaban Kamusoko, pamoja na kiungo kisheti kutoka Rwanda Haruna Niyonzima . Yanga inampango wa kuongeza mkataba na Thaban Kamusoko tu.
0 comments:
Post a Comment