728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, April 18, 2017

    Wachezaji Yanga SC wapewa siku tatu za mapumziko,wakirejea kuivaa Tanzania Prisons Jumamosi


    Paul Manjale,Dar Es Salaam.

    BAADA ya wachezaji wake 11 wa mwisho waliokuwa wamekwama nchini Algeria kutokana na kuchelewa ndege kuwasili alasiri ya leo,uongozi wa mabingwa watetezi wa ligi kuu bara,Yanga SC umetoa mapumziko ya siku tatu (3) kwa wachezaji pamoja na benchi lake zima la ufundi. 

    Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya klabu hiyo,Salum Mkemi amesema wameamua kutoa mapumziko hayo ili kutoa muda wa kutosha kwa wachezaji na watu wa benchi la ufundi kupumzika pamoja na kuwa karibu na familia zao baada ya kuwa nazo mbali kwa siku kadhaa.

    Mkemi ameongeza kuwa Yanga SC itarejea mazoezini siku ya Alhamisi kujiandaa na mchezo wao wa robo fainali ya kombe la kombe la FA dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya utakaochezwa Jumamosi ijayo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

    Wakati huohuo Mkemi ametoa onyo kwa vilabu vya ligi kuu baada ya kusema vijiandae kupokea maumivu kwani baada ya Yanga kutolewa kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika sasa hasira zake zote zimehamia kwenye michuano ya ligi kuu na ile ya FA ambao wao ni mabingwa watetezi.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Wachezaji Yanga SC wapewa siku tatu za mapumziko,wakirejea kuivaa Tanzania Prisons Jumamosi Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top