728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, April 25, 2017

    Hajji Manara awajia juu TFF , Soma alichoposti ndani




    Haji Manara

    Namshukuru Mungu kwa sasa masuala yangu binafsi ya kifamilia nimeyamaliza. 

    na naweza sema kitu, kwanza niwape pole nyie kwa haya yaliyonitokea, mimi si mtu ninayeamini uonevu si mtu ninayeweza kunyamaza nikiona haki inaporwa, si mtu mwenye moyo dhaifu wa kuogopa kukosoa pale panapopaswa kurekebishwa, na always ntabaki hivyo, Juzi Ijumaa jioni niliambiwa na ofisi yangu imekuja barua toka TFF, ikiniarifu kuna wito wa kunitaka nifike Karume kusikiliza mashtaka dhidi yangu jpili ya jana asubuhi, wakati huo nikiwa zbar kwa masuala yangu ya kifamilia, na ofisi ikaiandikia Tff barua ya kuomba kusogezwa mbele kwa shauri hili hadi jnne ya kesho kwa kuwa ntakuwa nipo Dar Es Salaam. 

    Barua iliwafikia na binafsi nikaongea na Afred Lucas msemaji wao na akanijibu ameipokea yeye na imegongwa muhuri na katibu mkuu wa TFF keshaipata, kumbuka hiyo ni jioni ya Ijumaaa , Jumamosi  nikampigia Alfred kuulizia kikao hicho cha kamati kimepangwa lini,akanijibu jumatatu ya leo atanijibu, jana tena mkasikia mliyosikia,ni uharaka upi ilionao tff wa kushindwa kunipa haki ya kusikilizwa? natural justice nchi hii haitambuliki!!wahaini na wauaji nao pia husikilizwa,,iweje kwa mtuhumiwa ambae anapigia kelele haki ya mwajiri wake?

    kuna hoja dhaifu inajengwa kuwa nilipaswa nijibu binafsi barua ya Tff , hivi ningewezaje kuijibu barua wakati sikuwepo Dar na sikuwa nimeiona na vipi klabu yangu isiwe na haki ya kunijibia barua, wakati leo imepokwa haki ya kutokuwa na msemaji? na hivi Tff hawajui kuwa mimi nilikuwa naongea kwa niaba ya ofisi na klabu yangu?

    Nikija sababu za kunifungia nimejiuliza ni kaka yangu huyu Msemwa aliyekuwa anasoma hii hukumu? nimemuona kwa Millard Ayo, anasoma hukumu ilio kinyume na hati ya mashtaka, hati yao ina makosa mengine na hukumu pia nyingine, ni aina ya hukumu katili zaid kwa vwango vya mpira wetu, ila nawaambia Tff Haji hajawahi kuwa dhaifu wa moyo, anaweza kuwa dhaifu wa kiwiliwili, lakini nna moyo wa Simba, ntapambana kwa kiwango cha juu sana, ntadai haki yangu na ya mwajiri wangu kwa viwango, na ntaziomba kamati zao zipokee rufaa yangu na kukaa kwa uharaka huu walionifanyia, na nipewe haki ya kusikilizwa,nisihukumiwe kishabiki wala kwa chuki, na nawahakikishia kikao kitakachokaa na kikiweza kunithibitishia niliosema si sahihi na nimeyatunga na yamepotosha, ntakubali adhabu hata ya kufungiwa maisha kujihusisha na mchezo huu ulionilea na kunisomesha. 

    Mwisho niwaombe fans wetu watulie tukisubiri hizo barua zao, yangu bnafasi na ya klabu. 


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Hajji Manara awajia juu TFF , Soma alichoposti ndani Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top