728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, April 16, 2017

    Hizi hapa habari 13 za usajili kutoka barani Ulaya Jumapili ya leo April 16,2016


    Yacine Brahimi


    Brahimi:Arsenal imewaweka juu ya orodha yake ya matamanio ya kuwasajili winga wa Porto,Yacine Brahimi, 27 na kiungo wa Schalke Max Meyer, 21,ikiwa nyota wake wawili Alexis Sanchez na Mesut Ozil wataamua kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.(Sun on Sunday)

    Costa:Chelsea itamruhusu mshambuliaji wake Mhispania,Diego Costa kuondoka Stamford Bridge na nafasi yake itazibwa na Alvaro Morata wa Real Madrid.Costa,28,bado anawindwa na miamba wa China,Tianjin Quanjian ambao mwezi Januari walitaka kumsajili kwa dau la £90m.(Sunday Express)

    Verratti:Marco Verratti ameripotiwa kuwa ataomba kuihama Paris
    Saint-Germain ikiwa klabu hiyo ya Ufaransa itashindwa kutenga bajeti ya maana kwa ajili ya kufanya usajili wa nguvu katika dirisha lijalo la usajili barani Ulaya.(Sunday Express)

    Ranieri:Watford imeripotiwa kuwa na mpango wa kumwajiri kocha wa zamani wa Leicester City  Muitaliano,Claudio Ranieri kwa ajili ya kuchukua mikoba ya Walter Mazzarri atakayefukuzwa mwishoni mwa msimu huu.(Sunday Express)

    Isco:Kiungo wa Real Madrid Isco Alcoron,24,amesema angependelea kubaki klabuni hapo licha ya kuwepo kwa uvumi kuwa atauzwa wakati wa dirisha lijalo la usajili barani Ulaya .(AS)

    Hazard:Eden Hazard amemwambia mchezaji mwenzie klabuni Chelsea,Michy Batshuayi, 23, kutafuta klabu mpya ya kuichezea ikiwa ataendelea kukosa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Antonio Conte.(DH, via Metro)

    Pochettino:Kocha wa Tottenham,Mauricio Pochettino amesema klabu hiyo haitajiingiza kwenye mbio za kuifukuzia saini ya mshambuliaji wa Real Madrid,Alvaro Morata.(Daily Star Sunday)

    Bartley:Burnley imesema itamsajili beki wa kati wa Swansea City,Kyle Bartle anayecheza kwa mkopo Leeds United ikiwa beki wake wa kati Michael Keane,24, ataondoka klabuni hapo katika dirisha lijalo la usajili barani Ulaya.(Sun on Sunday)

    Tierney:Beki wa kushoto wa Celtic Kieran Tierney, 19,ameripotiwa kuvutiwa zaidi na mpango wa kujiunga na Manchester United kuliko vilabu vya Arsenal na Tottenham ambavyo pia vimeonyesha nia ya kuitaka huduma yake. (Manchester Evening News)

    Jokanovic:West Ham itamchukua kocha wa Fulham,Slavisa Jokanovic pindi itakapoachana na kocha wake wa sasa,Slaven Bilic ifikapo mwishoni mwa msimu huu.(Sunday Express)

       
                                                      Max Meyer

    Onyekuru:Mshambuliaji kinda wa Eupen ya Ubelgiji,Mnigeria Henry Onyekuru amefichua kuwa siku moja angependa kujiunga na Arsenal ili kufuata nyazo za shujaa wake Mfaransa,Thierry Henry ambaye alifanikiwa sana klabuni hapo.Onyekuru,19,msimu huu tayari ameifungia Eupen mabao 12 na kupika mengine saba.(Sunday Mirror)

    Barkley:Kocha wa Manchester United Mreno, Jose Mourinho anajiandaa kufanya usajili wa kushitukiza kwa kumsajili kiungo wa Everton,Ross
    Barkley ambaye amedokeza kuwa angependa kuondoka Goodson Park na kujiunga na timu ambayo itampa nafasi ya kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao.(Sunday Mirror)

    Kompany:Vilabu vya West Ham na Everton kwa pamoja vimeonyesha nia ya kutaka kumsajili nahodha wa Manchester City, Vincent Kompany ambaye kuna uwezekano mkubwa akauzwa mwishoni mwa msimu huu kutokana na kuendelea kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.(Sunday Mirror)


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Hizi hapa habari 13 za usajili kutoka barani Ulaya Jumapili ya leo April 16,2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top