London, England.
ARSENAL imeungana na Chelsea kutinga fainali ya michuano mikongwe ya kombe la FA baada ya jioni ya leo kuifunga Manchester City mabao 2-1 katika mchezo mkali wa nusu fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Wembley jijini London.
Mabao yaliyoipeleka Arsenal fainali yamefungwa na Nacho Monreal pamoja na Alexis Sanchez huku bao la Manchester City likifungwa na Sergio Kun Aguero.
Fainali ya kombe la FA itachezwa Mei 27 mwaka huu kwenye dimba la Wembley kwa Arsenal na Chelsea kupambana.
0 comments:
Post a Comment