Lubumbashi,Congo DR
TP Mazembe imemteua mlinzi na nahodha wake wa zamani,Pamphile Mihayo Kazembe kuwa kocha wake mkuu mpya.
Kama ambavyo vilabu vya Ajax na Barcelona vimekuwa na kawaida ya kuwapa nyota wao wa zamani nafasi za kufundisha vikosi vyao,TP Mazembe nayo imempa nafasi Mihayo kuchukua mikoba ya Mfaransa,Thierry Froger aliyetimuliwa kazi baada ya mabingwa hao mara tano wa Afrika kuondolewa mapema kwenye kinyang'anyiro cha michuano ya klabu bingwa Afrika.
Kabla ya kupewa jukumu hilo Mihayo alikuwa akihudumu kama kocha wa muda tangu mwishoni mwa msimu uliopita akichukua mikoba ya Mfaransa,Hubert Velub aliyejiuzulu.
Akiwa mchezaji,Mihayo aliiwezesha TP Mazembe kutwaa vikombe viwili vya klabu bingwa Afrika mwaka 2009 na 2010.Akiwa kocha wa muda ameiwezesha miamba hiyo kufuzu nusu fainali ya kombe la shirikisho Afrika baada ya kuifunga JS Kabylie ya Algeria mabao 2-0.
0 comments:
Post a Comment