Rabat,Morocco.
TIMU ya taifa ya soka ya Tanzania ya vijana wa chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys leo Jumanne itashuka tena dimbani jijini Rabat nchini Morocco kucheza mchezo wa marudiano wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya vijana ya Gabon.
Serengeti Boys ambayo imeweka kambi jijini Rabat kwa takribani wiki tatu sasa ikijifua tayari kwa michuano ya vijana ya Afrika (AFCON) itakayofanyika mwezi ujao huko nchini Gabon,inaingia katika mchezo wa leo ikiwa na kumbukumbu ya kuifunga Gabon mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa Jumamosi iliyopita.
Baada ya mchezo huo Serengeti Boys itaendelea na mazoezi yake jijini Rabat kabla ya Alhamis Aprili 27 kuelekea nchini Cameroon ambapo itaweka kambi yake ya pili.
Ikiwa nchini humo,Serengeti Boys itacheza michezo miwili ya kujipima nguvu na wenyeji wao Cameroon Aprili 30 na kurudiana Mei 3 kabla ya Mei 7 kuelekea nchini Gabon tayari kwa kimuhemuhe cha michuano ya AFCON ambayo itaanza kutimua vumbi lake Mei 14 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment