Paris,Ufaransa.
MSHAMBULIAJI mahiri wa Uruguay,Edinson Cavani amesaini kandarasi mpya ya miaka miwili ya kuendelea kuitumikia klabu yake ya Paris Saint-Germain mpaka mwaka 2020.
Cavani,30,ambaye amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu akipachika mabao 44 kwenye michezo 43 amesaini kandarasi hiyo mpya baada ya Paris Saint-Germain kukubali matakwa yake.
Cavani alijiunga na Paris Saint-Germain Julai 2013 akitokea Napoli ya Italia kwa ada ya €50m.Mpaka sasa ameifungia miamba hiyo mabao 125 katika michezo 192.
0 comments:
Post a Comment