Ismailia,Misri.
Kampala City Capital Authority (KCCA) ya Uganda imekuwa timu ya kwanza kutoka Afrika Mashariki kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya Jumamosi usiku kuing'oa Al Masry ya Misri kwa penati 4-3 katika mchezo mkali wa marudiano uliochezwa huko Ismailia,Misri.
Timu hizo zililazimika kupigiana mikwaju ya penati baada ya kupata matokeo sawa ya 1-1.Matokeo hayo yakiwa ni ya jumla yaani aggregate.Katika mchezo wa kwanza uliochezwa huko Uganda,KCCA ilishinda kwa bao 1-0 kabla ya Jumamosi usiku kufungwa bao 1-0 lililofungwa na Ahmed Gomaa.
kipa wa KCCA,Benjamin Ochan aliibuka shujaa kwenye mchezo huo baada ya kudaka mikwaju miwili ya penati ya Said Mourad na Ahmed Ayman Mansour na kisha kufunga mkwaju mmoja.Penati za KCCA zimefungwa na Geofrey Sserunkuma,Muzamiru Mutyaba,Timothy Dennis Awany na Benjamin Ochan mwenyewe.
Katika mchezo mwingine wa michuano hiyo Zesco United nayo imefuzu hatua ya makundi baada ya kuifunga Enugu Rangers ya Nigeria mabao 3-0 kwenye dimba la Levy Mwanawasa kwa mabao ya John Ching’andu aliyefunga mara mbili na Mkenya Jesse Jackson Were aliyefunga bao moja.
0 comments:
Post a Comment