Calabar,Nigeria.
ZAIDI ya mashabiki 30 wa soka nchini Nigeria wanahofiwa kufa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya kibanda walichokuwa wakikitumia kufuatilia mtanange wa Europa Ligi kati ya Manchester United na RSC Anderlecht kukumbwa na hitilafu ya umeme.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku wa kuamkia leo huko Atimbo,kusini mashariki mwa jimbo la Calabar ambapo mashuhuda wa tukio hilo wamedai chanzo cha tukio hilo kimetokana na hitilafu ya umeme iliyosababishwa na waya uliochomoka kwenye nguzo na kudondokea kibandani hapo.
0 comments:
Post a Comment