Rabat,Morocco
TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys jana Jumamosi usiku ilifanikiwa kuwafunga wenyeji wa michuano ya AFCON ya vijana,Gabon mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa huko mjini Rabat nchini Morocco.
Mabao ya Serengeti Boys katika mchezo huo uliochezweshwa wa maamuzi kutoka Morocco,yametiwa kimiani na Kelvin Nashon Naftali katika dakika ya 18 na Ibrahim Abdallah Ally katika dakika ya 75.
Serengeti Boys imeweka kambi ya mwezi mmoja nchini Morocco kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, zinazotarajiwa kuanza Mei 14 hadi 28,mwaka huu nchini Gabon.
Serengeti Boys itakuwa kambini mjini Rabat hadi Mei 1, mwaka huu itakapowenda Younde, Cameroon kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya wenyeji Mei 3 na 6, mwaka huu.
Mei 7 timu hiyo itakwenda Gabon ambako imepangwa kundi B pamoja na timu za Ethiopia, Niger na Angola,wakati Kundi A lina timu za wenyeji, Gabon, Guinea,Cameroon na Ghana.
0 comments:
Post a Comment