Madrid, Hispania.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ufaransa,Antoine Griezmann usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kuandika jina lake kwenye vitabu vya kumbukumbu za kudumu vya ligi ya La Liga baada ya kufikisha mabao 100.
Griezmann amefikisha idadi hiyo ya mabao baada ya bao lake la dakika ya 73 kuipa Atletico Madrid ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Espanyol.
Griezmann anakuwa Mfaransa wa pili kufikisha mabao 100 La Liga nyuma ya mshambuliaji wa Real Madrid,Karim Benzema mwenye mabao 120.
Ikumbukwe Griezmann amefikisha mabao hayo 100 baada ya kuifungia klabu yake ya zamani ya Real Sociedad mabao 40 kisha mabao 60 akiwa na Atletico Madrid.
0 comments:
Post a Comment